Sunday, September 17, 2017

UHAKIKI TOKA NACTE TAYARI UMEKAMILIKA


 Image result for nacte

Uhakiki wa Udahili wa Wanafunzi wanaotarajia kujiunga kwenye vyuo vya Serikali, Afya na Ualimu Umekamilika, Unaweza kuangalia matokeo ya uchaguzi huu kupitia kwenye kurasa binafsi kwa kubofya hapa, Mfumo utafunguliwa tena hivi karibuni kuruhusu awamu ya pili kwa waombaji wapya na wale wenye sifa lakini hawakuchaguliwa. Asante.

Wednesday, May 24, 2017

TAARIFA KWA UMMA TOKA JESHI LA KUJENGA TAIFA.



    Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), limechagua vijana waliohitimu Elimu ya Sekondari Kidato cha Sita kwa mwaka 2017, kutoka Shule zote za Tanzania Bara kuhudhuria mafunzo ya JKT kwa Mujibu wa Sheria.
 Sanjari na Uchanguzi huo, JKT limewapangia Makambi watakayokwenda kupatiwa mafunzo kwa muda wa miezi mitatu na wanatakiwa kuripoti Makambini kuanzia tarehe 25 – 30 Mei 2017.
 Vijana waliochanguliwa, wamepangiwa katika kambi za JKT Rwamkoma – Mara, JKT Msange – Tabora, JKT Ruvu – Pwani, JKT Makutopora – Dodoma, JKT Mafinga – Iringa, JKT Mlale – Ruvuma, JKT Mgambo na JKT Maramba – Tanga, JKT Makuyuni – Arusha, JKT Bulombora, JKT Kanembwa na JKT Mtabila – Kigoma.
 Aidha, wahitimu wenye ulemavu wa kuonekana kwa macho (physical disabilities) wanatakiwa kuripoti kambi ya JKT Ruvu iliyopo Mlandizi mkoani Pwani ambayo ina miundombinu ya kuhudumia watu wa jamii hiyo.

JKT linawataka vijana hao kuripoti wakiwa na vifaa vifuatavyo:
  1. Bukta ya rangi ya ‘Dark blue’ yenye mpira kiunoni (lastic), iliyo na mfuko mmoja nyuma, urefu unaoishia magotini, isiyo na zipu.
  1. Raba za michezo zenye rangi ya kijani au blue.
  1. Shuka mbili za kulalia zenye rangi ya blue bahari
  1. Soksi ndefu za rangi nyeusi.
  1. Nguo za kuzuia baridi kwa waliopangiwa mikoa yenye baridi.
  1. Track suit ya rangi ya kijani au blue.
  1. Nauli ya kwenda makambini na kurudi majumbani.
Mkuu wa JKT anawakaribisha Vijana wote waliochaguliwa ili waweze kujiunga na Vijana wenzao katika kujifunza Uzalendo, Umoja wa Kitaifa, Stadi za kazi, Stadi za maisha na Utayari wa kulijenga na kulitumikia Taifa letu.
KUONA MAJINA BONYEZA HAPA >>>> @IBUU<<<<<

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Habari na Uhusiano,
Makao Makuu ya JKT,
Tarehe 22 Mei 2017

Monday, May 22, 2017

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU UDAHILI WA WANAFUNZI WA ASTASHAHADA NA STASHADA KATIKA PROGRAMU MBALIMBALI KWA MWAKA WA MASOMO 2017/2018

BARAZA LA TAIFA LA ELIMU YA UFUNDI
(NACTE)


TAARIFA KWA UMMA KUHUSU UDAHILI WA WANAFUNZI WA ASTASHAHADA NA STASHAHADA KATIKA PROGRAMU MBALIMBALI KWA MWAKA WA MASOMO 2017/2018

Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) ni chombo kilichoanzishwa kwa sheria ya Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi, Sura 129, ili kusimamia na kuratibu utoaji wa mafunzo ya elimu ya ufundi nchini. Sheria hii inazitaka Taasisi zote zinazotoa elimu ya ufundi kusajiliwa kabla ya kuanza kuendesha mafunzo yoyote. Baraza pia huidhinisha mitaala kabla haijaanza kutumika. Hivyo taasisi zote haziruhusiwi kuanza kutoa mafunzo yoyote bila kibali maalumu kutoka Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE).

Baraza linapenda kuwataarifu wadau wa sekta ya Mafunzo ya Ufundi na Umma kwa ujumla kuwa udahili na uchaguzi wa wanafunzi kwa ajili ya masomo ya Astashahada na Stashahada mbalimbali yanayotolewa na vyuo vyote hapa nchini, utafanyika moja kwa moja vyuoni, isipokuwa kozi za afya na ualimu zinazotolewa na  vyuo vya Serikali tu. Hivyo maombi yote ya nafasi za masomo yatumwe kwenye chuo husika.

 Udahili wa kozi za Afya na Ualimu katika vyuo vya Serikali  utaratibiwa na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto; na Wizara ya Elimu, Sayansi na Tekinolojia kwa kushirikiana na Baraza (NACTE). Hivyo maombi ya Udahili kwa kozi za Afya na Ualimu kwa vyuo vya serikali tu yatumwe kwa njia ya mtandao kupitia tovuti ya NACTE (www.nacte.go.tz) au kupitia vyuo husika vya Afya na Ualimu ambavyo vitashughulikia maombi hayo na kufanya udahili kwa njia ya mtandao kupitia ‘Institutional Panel’ zao.

Aidha vyuo vyote vitatangaza au kuwafahamisha moja kwa moja waombaji majina ya watakaochaguliwa kujiunga na kozi mbalimbali; na wale wa kozi za Afya na Ualimu watatangazwa na Wizara husika na kupitia tovuti ya NACTE.

Baraza linapenda pia kuwafahamisha kuwa Vyuo vitaanza kupokea maombi ya udahili wa wanafunzi kuanzia tarehe 15 Mei, 2017 hadi tarehe 20 Agosti, 2017. Majina ya waliochaguliwa yatatangazwa tarehe 14 Septemba, 2017. Masomo kwa mwaka wa masomo 2017/2018 yanatarajiwa kuanza rasmi tarehe 25 Septemba, 2017.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA KATIBU MTENDAJI
BARAZA LA TAIFA LA ELIMU YA UFUNDI (NACTE)
TAREHE: 10/05/2017

NACTE: THE CENTRAL ADMISSION SYSTEM FOR ACADEMIC YEAR 2017/2018 IS ON

THE NATIONAL COUNCIL FOR TECHNICAL EDUCATION (NACTE)ONLINE APPLICATION AND VERIFICATION SYSTEM

NACTE: KUFUNGULIWA KWA MFUMO WA PAMOJA WA UDAHILI 2017/18

Please read carefully the information in this page before attempting to do anything. 

Welcome to Online Application Verification System for Certificate and Diploma.
 
The System allows you to apply for Admission into Further Education for academic year 2017/2018.
Currently Available Application Categories:-
- Admission into Certificate/Diploma
Health and Allied Sciences (Including Community Health, Health Records etc) :- Deadline 20/08/2017

  
                          CLICK HERE TO READ MORE AND APPLY

Saturday, April 29, 2017

HII HAPA ORODHA YA WATUMISHI WA UMMA WENYE VYETI FEKI

Nimekuwekea hapa orodha ya watumishi wenye vyeti feki kuipata bonyeza hapa  @ibuu
Pia tunaweza kukuangalizia jina lako kwa kasi ya ajabu cha kufanya tuma shillingi 1000 kwenda namba 0757504082,Na tutakujibu ndani ya dakika 2
Jamii yangu team

Wednesday, April 12, 2017

HAYA HAPA MAJINA AJIRA MPYA ZA WALIMU 2016/2017


Hatimaye serikali ya jamhuri ya Muungano wa Tanzania imetangaza majina ya walimu walioajiriwa mwaka 2016/2017.


KUONA MAJINA YA WALIMU WATAKAOFUNDISHA KIDATO CHAKWANZA HADI CHA NNE AMA CHA TANO NA SITA
Tafadhali bonyeza hapa @Ibuu.co.tz

pia  bonyeza hapa @Ibuu kupata majina kwa wale walim wa kidato cha kwanza hadi cha nne

Thursday, March 30, 2017

Medical Officer


Details
Employer Name: Peace Corps
Organization Type: NGO
Role: Management
Position Type: Full Time
Location: Dar Es Salaam
                    Other Dar es Salaam District
Application Deadline: 19-04-2017
Listed on: 29-03-2017
Description