Thursday, March 9, 2017

NDUGU WA MCHUNGAJI GWAJIMA AIBUKA,AONGEA HAYA

Mwanasheria Methusela Gwajima Mdogo wa Askofu  wa kanisa la Ufufuo na Uzima Dk JosephatGwajima leo ameibuka na kuwapingana  wanaohoji kuhusu elimu ya mkuu wa mkoa wa Dar Es Salaam,RC Paul Makonda, na kuuliza walikuwa wapi kabla. Methusela Gwajima amepingana na kinachofanywa na kaka yake Askofu Gwajima kuifanya elimu ya RC Makonda kuwa ajenda kanisani,amesema kuwa kama kaka yake anaona alionewa aeende Mahakamani.Amesema kuwa mjadala huu umeizima ajenda ya dawa za kulevya jambo ambalo si sahihi.Amesema anamwambia kaka yake aache kutumika na kuhoji ni kina nani wanamtuma askofu Gwajima.Amewataka watanzania wazalendo kuepuka kujiingingiza kwenye ajenda ya vyeti